7 Julai 2025 - 23:09
Source: Parstoday
Ayatullah Khamenei aongoza majlisi ya maombolezo ya usiku wa A'shura mjini Tehran

Shughuli ya maombolezo ya usiku wa Ashura ilifanyika jioni ya jana Jumamosi katika Husseiniya ya Imam Khomeini mjini Tehran, ikihudhuriwa na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei na mkusanyiko mkubwa wa watu wa matabaka mbalimbali.

Kaulimbiu za muqawama na kusimama kidete dhidi ya dhulma kutokana na mashambulizi ya siku 12 za Israel dhidi ya Iran ziliangaziwa zaidi katika hotuba ya Hujjatul Islam Masoud Ali aliyehutubia majlisi hiyo na kusisitiza umuhimu wa mafunzo na ibra za mapambano na kuuawa shahidi Imam Hussein bin Ali (AS) katika siku ya A'shura mwaka 61 Hijria katika medani ya Karbala.

Hujjatul Islam Masoud Ali ametaja mapambano ya Iran kama sehemu ya harakati pana ya kimataifa, na kwamba Iran ya Kiislamu ni "mhimili" wa kambi ya kimataifa chini ya uongozi wa Ayatullah Ali Khamenei dhidi ya "kambi ya batili" inayoongozwa na Uzayuni wa kimataifa.

Ameongeza kuwa: "Kutokana na mafundisho ya A'shura, taifa la Iran kamwe halitasalimu amri kwa kambi ya batili, kwa sababu limeifanya kauli mbiu ya 'Kamwe kudhalilishwa' kama mwongozo na dira yake." 

Ayatullah Khamenei aongoza majlisi ya maombolezo ya usiku wa A'shura mjini Tehran

Wairani katika mji mkuu Tehran, majiji, miji na vijiji vyote nchini jana Jumamosi walikusanyika misikitini, katika na vituo vya kidini, na barabarani katika shughuli ya siku ya tasu'a ya kuomboleza mauaji ya Bwana wa Mashahidi, Imam Hussein bin Ali AS.

Waombolezaji katika kona zote za Iran wametangaza kwa sauti kubwa utiifu wao kwa wanamapambano wa Karbala, huku wakijibari na kujiweka mbali na maadui wa Uislamu na wa Ahlul Bayt wa Mtume Muhammad SAW.

Your Comment

You are replying to: .
captcha